About Ishi Kistaa

Ishi Kistaa ni kampeni ya kitaifa ya burudani iliyoanzishwa ili kuwapa nafasi mashabiki, wapenzi wa sanaa za ndani na wasanii wa tasnia kubwa za  burudani ndani ya Bongo, Muziki (Bongo Fleva) na Filamu (Bongo Movie) kuweza kukutana pamoja na kubadilishana mawazo huku mashabiki wakipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kutoka kwa wasanii wawapendao.

Kampeni hii inaendeshwa kupitia kipindi cha Televisheni cha ISHI KISTAA ambacho kwa sasa kiko kwenye msimu wa kwanza wa Ishi Kistaa

Mbali ya kukutana na wasanii na kushinda zawadi mbalimbali mashabiki pia watakuwa wakipata habari zinazowahusu wasanii hao na kuongeza uwezekano wa kushinda nafasi ya kukutana nao.

Habari za wasanii mastaa hutumwa kila siku kwa mashabiki wao kupitia ujumbe mfupi wa maneno (sms).

Pia mashabiki wanaweza kufuatilia habari zinazowahusu mastaa wao kupitia tovuti: Ishi Kistaa na mitandao ya kijamii: Facebook ,  Twitter na Instagram na kutoa maoni mbalimbali kwa wasanii hao.

Ili shabiki aweze kupokea ujumbe wa msanii anayempenda na kushinda nafasi ya kukutana nae na kupata zawadi nyinginezo atapaswa kutuma neno STAA kwenda namba 15670.