Abdu Kiba afunga ndoa visiwani Zanzibar

0
768

Baada ya mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba kufunga ndoa jijini Mombasa, mdogo wake Abdukiba naye amefunga ndoa visiwani Zanzibar.

Abdu Kiba amefunga ndoa pia na moja ya mtu wake wa karibu na kufanikiwa kuongeza idadi ya wanawake katika familia yao.

Kwa upande wake msanii anayejulikana kwa jina la H Baba ambaye ni mtu wa karibu na kina Ali kiba ameweka wazi kuwa Abdu kiba leo amefunguka ndoa na kumtakia kheri kwenye siku yake hiyo muhimu katika maisha yake.

“Hongera sana Abdu Kiba kwa kuchukua jiko lako Allah akulindie ndoa yako, jambo la kheri uja na kheri zake karibu chama la waliompendeza Mungu kwani kuoa ni jambo la kheri,”.

Hata hivyo, Ali kiba na Abdu Kiba wanadhaniwa kuwa huenda wanaweza kufanya sherehe ya pamoja April 29, 2018 jijini Dar es Salaam ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi lao la kufunga ndoa.

LEAVE A REPLY