Abdu Kiba adai hasumbuliwi na skendo za mtandaoni

0
274

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdu Kiba amesema kuwa maisha yake ya muziki hayasukumwi na skendo za mitandao ya kijaami, badala yake ataendelea kutumia kipaji chake na kutoa kazi zenye viwango.

,Kiba alisema wasanii wengi wanaopenda skendo hawajiamini na wao ndio chanzo cha kushusha thamani ya muziki nchini.

“Muziki ni maisha yangu na kazi inayonipa fedha za kujikimu mimi na familia yangu, napenda kutoa kazi zenye viwango ndio maana mashabiki wananipenda na kuendelea kufuatilia kazi zangu.

“Katika vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo, mambo kama haya huwa ni sababu ya kushusha thamani ya mtu na kazi yake,”.

LEAVE A REPLY