Makumi wauawa Syria kwenye shambulio la majeshi ya washirika

0
144
Smoke rises after a U.S.-led coalition airstrike on Kobani, Syria, Monday, as seen from the Turkish side of the border. Kurdish fighters say they're making progress against ISIS in the area.

Watu 56 ambao ni raia wameuawa kwenye shambulio la anga lililofanywa na majeshi washirika yanayoongozwa na Marekani karibu na ngome ya kundi la IS kaskazini mwa Syria.

Waangalizi wa haki za binadamu wa Syria wameripoti kuwa wakazi wengi wameonekana wakikimbia katika mji wa Tokhar baada ya eneo hilo kushambuliwa.

Wakati huohuo mtandao wa wanaharakati wa upinzani umedai kuwa idadi ya watu waliofariki ni 90 na sio 56 kama ilivyoripotiwa na kundi la waangalizi ingawa Serikali ya Syria na majeshi ya muungano hawajatoa taarifa yoyote kuhusu shambulio hilo na madhara yake.

3rd Content - INSIDE IMAGE

LEAVE A REPLY