Nyimbo za Otile Brown zafutwa Youtube

0
54

Nyimbo kadhaa za wasanii maarufu wa muziki nchini Kenya zimedaiwa kutoweka kwenye chaneli za wasanii husika kwenye mtandao wa Youtube ambapo bado haijabinishwa nini kimepelekea hilo.

Miongoni mwa Video za muziki zinazodaiwa kutoweka kwenye mtandao huo ni pamoja na Dusuma ya Otile Brown, Maombi na Kolo za Nadia Mukami na Radio Love ya Arrow Bwoy.

Kwenye mitandao ikiwemo twitter na Instagram, baadhi ya mashabiki wakiwemo mashabiki wa wasanii hao wamehoji juu ya hilo lililokumba kazi za wasanii hao.

Baadhi ya mashabiki kwenye jumbe tofauti wameonesha shauku ya kutaka kujua ni nani au nini kinaendelea kiasi cha kutoweka kwa kazi hizo.

LEAVE A REPLY