Ushauri wa Profesa Jay kwa wasanii

0
18

Baada ya kuachia ngoma yao mpya inayoitwa BABA ambayo ni collabo ya Stamina na Profesa Jay wakimshirikisha One Six, sasa Profesa ameeleza darasa walilotoa kwenye kiwanda cha muziki bongo.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Profesa amesema sio lazima kuimba matusi na mambo ya kitandani na kuna nafasi kubwa ya kukiokoa kizazi.

SHULE YA BURE

Sio lazima kila siku uimbe MATUSI na Mambo ya kitandani ili Wimbo wako uwe mkubwa na upendwe, Bali unaweza kuimba wimbo wenye mafunzo mema kwa jamii na Wadau wakakushika mkono kwa kiwango cha juu kabisa, Kwa Pamoja tunaweza tukakiokoa KIZAZI hiki.

BABA ni ngoma ambayo inafanya vizuri sana kwa hivi sasa ambapo kupitia mtandao wa YouTube ndio video inayotazamwa zaidi tangu ilipotoka ikiwa inashika namba moja kwa kuwa na watazamani zaidi ya laki tisa.

LEAVE A REPLY