Muonekano mpya wa Rayvanny wazua gumzo

0
62

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny anadaiwa kubadilika kidogokidogo kila kukicha kutoka kwenye ule mwonekano wake wa kiume na sasa anatia shaka kiasi cha kuibuliwa skendo nzito kutokana na mapigo yake ya kike.

Tangu alipodaiwa kuachana na aliyekuwa mzazi mwenzake Fahyvanny aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydan, amekuwa hasomekisomeki huku mwonekano wake wa kike ukizua maswali mengi.

Rayvanny alianza kutupia picha zikimuonesha akiwa amevaa mawigi ya wanawake kichwani, huku mwenyewe akitamba kuwa ni mwonekano mpya.

Mwonekano wake wa akiwa ametengeneza nywele kama mwanamke, uliibua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakimtolea maneno ya kashfa.

Kwa upande wake Rayvanny amesema kuwa, hakuna lolote zaidi ya mtindo mpya wa kiume wa nywele zake na kwamba, umekuwa ni utaratibu wake wa kuzibadilisha mara kwa mara.

Baadhi ya mashabiki wamemtaka Rayvanny kurudi kwenye fasheni yake ya zamani ya virasta, kwani ilikuwa ikimpendeza zaidi kuliko hii ambayo inamsababishia kutiliwa shaka.

LEAVE A REPLY