Jide atangaza ujio wa albam yake mpya ‘Woman’

0
198

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ ametangaza ujio wa albam yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Women’ itakayotoka mwezi Machi mwaka huu baada ya kukamilika.

Lady Jay Dee ametangaza ujio wa albam hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuposti picha ya kava ya albam hiyo ambayo itatoka baada ya kukamilika ambapo nyimbo kwenye albam hiyo zimefanywa na watayarishaji tofauti nchini.

Mwanamuziki huyo amewaomba mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa kuipokea albam hiyo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kuachia albam.

Pia Jide anatarajia kufanya concert kwa ajili ya kuitangaza albamu hiyo pamoja na kuipromote kwa mashabiki wake ambao walikuwa wanamisi albam ya mkali huyo.

Jide ni mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva ambaye anaendelea kufanya vizuri hadi hivi sasa kutokana na ubora wa nyimbo zake ambazo zimeendelea kudumu hadi hivi leo.

 

LEAVE A REPLY