Zlatan kuwa ‘MUNGU’ wa Manchester United?

0
137

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, Zlatan Ibrahimovich amemjibu mshambuliaji wa zamani na staa wa klabu hiyo Eric Cantona kuwa hawezi kuwa mwana wa mfalme bali atakuwa Mungu wa Manchester.

Kauli ya Ibrahimovich imekuja baada ya nguli wa zamani wa Ufaransa, Cantona kumkaribisha Zlatan kwenye klabu hiyo na kupendekeza apewe jezi namba 7 ambayo ilikuwa ikivaliwa naye wakati alipokuwa akiichezea United.

Cantona alinukuliwa akisema:

‘Kuna mfalme mmoja tu Manchester, unaweza kuwa mwana mfalme ukipenda. Na, jezi namba 7 ni yako iwapo utapenda. Hiyo ndiyo zawadi yangu kwako. Mfalme ameshaondoka, uishi miaka mingi mwana mfalme’

Pamoja na pendekezo hilo la Cantona Zlatan amemjibu staa huyo kwa kumwambia kuwa yeye atakuwa mkubwa zaidi yake kwenye klabu hiyo.

‘Ninampenda Cantona na nimesikia kile alichokisema lakini sitakuwa mfalme wa Manchester, nitakuwa Mungu wa Manchester’

Ibrahimovich anatarajia kujiunga wenzake kwenye na kikosi cha Manchester United ili kuanza mazoezi ya pamoja lakini bado haijafahamika iwapo atasafiri na timu hiyo kwenda ziarani nchini China huku Morinho akiweka wazi kuwa staa huyo hatocheza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Manchester City na Borussia Dortmund.

LEAVE A REPLY