Rihanna kafuta onyesho Ufaransa

0
387

Staa wa Pop kutoka Marekani, Rihanna amefuta onyesho lake la muziki lililopangwa kufanyika usiku wa leo kwenye uwanja wa Allianz uliopo kwenye mji wa Nice ambapo mauaji ya watu 84 yametokea usiku wa kuamkia leo.

Tayari Rihanna alikuwa ameshafika nchini Ufaransa na wakati mauaji yanatokea alikuwa kwenye mji huo huo wa Nice ingawa wawakilishi wake wamethibitisha kuwa msanii huyo yuko salama.

Kwa sasa Rihanna anajipanga kufanya onyesho lake la Jumapili nchini Ujerumani kwenye mji wa Frankurt.

Rihanna mwenyewe amethibitisha taarifa za kufutwa kwa onyesho hilo kupitia mtandao wa Instagram.

rihanna1

LEAVE A REPLY