Kajala Masanja staa aliyepitia mengi mazito

1
1674
Kajala Masanja

Kajala Masanja ni mmoja wa mastaa wanaokubalika sana Tanzania hususani kwa wapenzi na mashabiki wa filamu za Bongo Movie.

Lakini wengi hawajui wapi ametoka na nani amemfikisha hapo.

Hii ni historia yake fupi ya kistaa.

Alizaliwa mwaka 1983,

Alisoma shule ya msingi Mbuyuni.

Mama Salma Kikwete ndiye aliyekuwa mwalimu wake wa darasa.

Ridhiwan na Miraji Kikwete walikuwa wanafunzi wenzake kwenye darasa moja na alikuwa anakaa nao dawati moja.

Amezaa na producer mwenye heshima kubwa Bongo, P-Funky Majani

Alianza kuwa staa wa filamu kwa msaada mkubwa wa Jacob Stephen (JB)

Mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya uvunjifu wa sheria za nchi.

Wema Sepetu alimlipia faini ya milioni 13 ‘cash’ na kumnusuru na kifungo hicho.

Urafiki wake na Wema uliingia dosari baad aya kupakaziwa kuwa anatembea na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema.

Alimlipia rapa Ibrahim Ayoub Mandingo aka ‘Country Boy’ pesa ya kwenda studio.

Mumewe, Faraja Chambo bado anatumikia kifungo cha miaka saba jela kwa kosa waliloshtakiwa pamoja na Kajala.

Alirudi kwa kishindo kwenye filamu na kuanzisha kampuni ya KAJALA ENTERTAINMENT na kufanya uzindumzi mkubwa wa filamu ya ‘Mbwa Mwitu’ kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Aliwakusanya wasanii wa komedi Mzee Onyango, Asha Boko na Senga na kuachia nao filamu yavichekesho.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY